Online Instagram Content ViewerGeneralsta
  1. Homepage
  2. storynzuriiplanet_com

#storynzuriiplanet_com photos and videos on Instagram

Medias attached with hashtag: #storynzuriiplanet_com on Instagram

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "Riwaya: MSITU WA SIRI 17
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA

Nlianza kuingiwa na amani na nikapata matumaini ya kurudi salama nyumb" at Kigamboni Bridge - 1861559093510900898

Riwaya: MSITU WA SIRI 17 Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA Nlianza kuingiwa na amani na nikapata matumaini ya kurudi salama nyumbani....mara kwambali naona watu wakikimbia ovyo kila mtu alipita njia yake......nilipotizama vizuri niliona kiumbe kile kimeingia kijijini kwetu... ****Endelea*** niliona wanakijiji wakikimbiahuku na huku kila mmoja alipita njia yake....niliingiwa na wasiwasi kuwa mama yanguatakuwa hatarini... nilitimua mbio kuelekea nyumbani..wakati nakimnia watu walinishanhaa..na kuniona kuwa nimechanganyiki wa...kwanini nikimbilie kule kwenye hatari wakati wao wanakimbia kwaajili ya kwenda kujificha ili waokoe usalama wa maisha yao"",, nilikimbia nikaingia mpaka ndani huku naita MAMA MAMA..... nilipotazama vizuri sikumuona mama nikaamua kutoka nje... nilisikitika sana kuona maiti nyingi za wanakijiji zikiwa zimetapakaa chini kama mchanga"" nilizitazama maiti zile ili niangalie kama miongoni mwa maiti zile huenda nikamuona mama yangu"" nilitazama maiti moja hadi nyingine kwa umakini zaidi...ndipo nikagundua kuwa hienda mama yangu bado Yuhai.....nikakimbia nisijue naelekea wapi....mara kwa mbali nilimuona mama nilifurahi sana nikaita mama kwa kupaza sauti lakini mama hakunisikia kutokana alichanganyikiwa juu ya kiumbe huyu wa ajabu kwa kuuwa watu... ****** nilipoona haisikii sauti yangu nikaamua kukimbia kuelekea ule upande aliokuwa mama...mara ghafla nilimuona kiumbe yule akimfuata mama alikuwa nyuma kama hatua kumi hivi...niliogopa sana...nikapaza sauti tena nikaita mama..mama..ghafla kiumbe kile kikaacha kumfaya mama kikasimama..kikageuza shingo kutazama ule upande niliopo...kiumbe yule alinitazama kisha akaendelea kumfuata mama...nilimuonea huruma mama yangu alikuwa anakimbia huku kanga zikimdondoka.... nikatoa mshale nikauweka kwenye upinde nikauvuta kwa nguvu zangu zote huku nikikumbuka mjomba paul alipokuwa akinifundisha jinsi ya kulenga kitu kikiwa mbali bila kukikosa...nilivuta kisha nikaachia mshale ule""" ulienda moja kwa moja mpaka kwenye mgongo wa kiumbe yule... #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lkn gh" at Dar es Salaam, Tanzania - 1850086677987416324

Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lkn ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama. Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama msafiri amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya. Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama. Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena msafiri amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama. Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia.. "Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mm ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe. Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena. FUNZO, Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe. *MUNGU ATUSAMEHE DHAMBI ZETU NA ATUWEKE HURU... AMIIN* #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 34 “Salim, Salma… majina na hata mlivyo mmeendana pia. Hongera Salma.” Aliongea Frank na wote wakafurahi." at Dar es Salaam, Tanzania - 1849280834681329433

MAPIGO YA MOYO 34 “Salim, Salma… majina na hata mlivyo mmeendana pia. Hongera Salma.” Aliongea Frank na wote wakafurahi. “ila nina ombi kwako Salim. Nakuomba uwe mwaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Salma. Huyu ni zaidi ya mke umepata. Ni zaidi ya mshauri pia ni zaidi wanawake bora ambao ulishawahi kukutana nao. Nitaumia sana nikisikia chochote kibaya kikitokea kwa huyu dada na wewe ndio ukawa msababishaji…. Ni hilo tu. Zaidi ya hayo nawatakia maisha mema na mungu awajaalie kizazi chema.” Aliongea Frank kwa uchungu moyoni lakini akiwa na tabasamu la plasitiki usoni. Wote walicheka na Salim alimyamyuka na kumpa mkono Frank. “nimekulewa. Nakuahidi kumpenda mpaka pumzi yangu ya mwisho wa uhai wangu.” Aliongea Salim na wote wakacheka. *********************** MWISHO************************* Natumaini mmepata elimu ndani ya burudani kutoka kwenye riway a yetu hii yenye hisia kali za mapenzi. Tujifunze kuridhika na wapenzi tulionao kwakua hujui kuwa umpendaye anaweza kubadilika baada ya kuchoka na visa vyako. Hakuna mwalimu wa mapenzi, kila mtu anajua na bwege wa mapenzi akierevuka humshinda professor na kumfanya kuwa matatani. Nyakati za kuumizana mioyo zimeshapita kama kweli utampata yule akupendaye. Maana kupenda sio kazi. Kazi ni unayempenda naye kukupenda kama unanyompenda wewe.. Kwa maoni, ushuri, na kama kuna mtu nimemkwaza kwa namna moja au nyingine, namuomba radhi na awe huru kuniambia kupitia in box na mimi nitajirekebisha. Maana na mimi ni binaadamu na kukosea nimeumbiwa. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 32

Macho ya Frank yalimuangalia na kujilaumu moyoni kumtesa msichana mzuri kama huyo.
“pole Frank.” Alio" at Dar es Salaam, Tanzania - 1849092395189093824

MAPIGO YA MOYO 32 Macho ya Frank yalimuangalia na kujilaumu moyoni kumtesa msichana mzuri kama huyo. “pole Frank.” Aliongea Lulu baada ya kumuona Frank akimuangalia. “ahsante, nimeshapoa baada ya kukuona tu.” Aliongea Frank na mama yake akaamua kuondoka kwakua alijua kuwa maongezi yanayoendelea yalikuwa hayamuhusu. “jamani nini tena kimekupata?” aliongea Lulu na kuonyesha ishara za kujali. “ni mitihani tu ya dunia .” aliongea Frank na kumuangalia Lulu kwa macho ya haya. “pole, mungu atakujaalia tu utapona.” Aliongea Lulu kwa hali ya kumuonea huruma Frank. “Lulu, najua kuwa kwa sasa unaweza kuwaza kwa nini nimeamua kukuita. Kusema ukweli, yule msichana niliyekuambia kuwa ni chaguo la moyo wangu. Ndio aliyenisababishia yote haya. Nilipotea njia. Ila kwakua yameshanikuta makuu ndio namekukubuka na kuona thamani yako ikiwa juu ya maisha yangu yaliyobakia. Ni wazi kuwa nakupenda ingawaje nilihisi utakuwa unanibana na kutokuwa huru kuwa na wasichana wengine. Ila nakuapia kuwa hivi sasa najutia kwa kila nilichokutendea na naomba uupokee moyo wangu mkosefu mbele yako wewe uliyejaa uvumilivu na mapenzi ya kweli juu yangu. Nakutamkia kauli kutoka moyoni kuwa nahitaji msamaha wako ili niwe wako kwa mara nyingine.” Aliongea Frank maneno hayo huku machozi yakimtoka na kumfanya Lulu mwenye machozi ya karibu kuanza kulia na yeye. “Frank hakuna mwanaume duniani niliyeiweka rehani roho yangu kwake kama wewe. Ulinifunba macho na kuwa sioni kwa penzi lako. Ni wewe ndiye uliyenifundisha na kunionjesha matamu ya mapenzi. Na ni wewe pia ndio uliyeniingiza kwenye dimbwi la wanaolilia mapenzi na kuniumiza moyo zaidi ya nilivyoumia siku waliyokufa wazazi wangu. Kwanini Frank uliamua kunitenda?? Kwanini uliamua kuninyanyasa kwa maneno yaliyonifanya nitamani kuupoteza uhai wangu??? Kwanini ulinitamkia kuwa mimi si chaguo lako?? Kwanini Frenk??” Aliongea Lulu maneno hayo kwa uchungu na kumfanya machozi yaliashiria uchungu uliopo moyoni mwake kumwagika kama maji. Hali hiyo nayo ilizidi kumuumizi Frank na kumfanya nae azidi kulia kwa uchungu. Kila akisemacho Lulu kilikua cha ukweli. “naomba unisamehe Lulu. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 31

Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu k" at Dar es Salaam, Tanzania - 1847775195719245136

MAPIGO YA MOYO 31 Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu kwa kumuamsha tena mtoto wao na kumpa uhai. Frank akiwa kitandani. Alikumbuka mbali sana toka anaanza mapenzi. Alikumbuka idadi ya wasichana waliokuwa wakilia na kumpigia magoti bila kosa lolote kumfanyia. Hakuamini kuwa mapenzi hayo hayo ambaye yeye alishayapatia yangewaza kumchenjia na kutaka kumpotezea uhai. Roho ilimuuma sana baada ya kumkumbuka Lulu. Hapo aliamini kuwa huyo ndio alikuwa chaguo lake ambalo mungu amemuandikia. Aliamini kile kilichomtokea ni adhabu kutoka kwa mungu kwa kumkataa mwanamke aliyekuwa na ndoto za kuishi naye bila kuhitaji kitu chochote kwake. Kuna wakati alikua anaamini kuwa toka aanze mapenzi, hakuna msichanana ambaye alikua na malengo naye kama Lulu. Mbali na kumtukana na kumdhalilisha, bado alikua anamuhitaji hata kwakua spare tyre. Taratibu moyo uliokufa ulianza kurudisha matumaini baada ya picha ya Lulu kuganda ubongoni. “mama , naomba muite Lulu aje kuniona.” Aliongea Frank baada ya mama yake kuletea chakula cha mchana. “halafu sijamuona siku nyingi sana huyo msichana na hata nyumbani haji kuni salimia kama zamani. Nitamuonea wapi mimi?” aliongea mama yake Frank kwa sauti ya utaratibu. “ni muhimu sana mama, nenda hata kwao.” Aliongea Frank na mama yake akakubali kufanya hivyo. Saa moja usiku, mama yake Frank aliwasili hospitali akiwa ameongozana na Lulu. Walifika mpaka kwenye kitanda cha Frank ambaye alikuwa amelala muda huo. Lulu alishangaa kumuona Frank akiwa na bandeji mwili mzima. Ilikuwa si rahisi kumtambua kwa haraka kwa jinsi alivyoviringishwa bandeji hio mpaka usoni na kuacha mdomo, Pua na macho tu. Mama yake Frank alimuamsha taratibu Frank. Alipoamka, alistaajabu Frank kumuona Lulu akiwa analengwa lengwa na machozi baada ya kumuona. Kingine kilichomshangaza ni jinsi Lulu alivyo vaa. Alikua kavaa nguo ndefu na kutupia ushungi aliojitanda vizuri. Muonekana wake ulizidi kuwa mzuri. Alikuwa kanenepa kiasi na kufanya Shape yake kuongezeka na kuwa bomba zaidi. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 30

Bila kuchelewa, wale wengine walianza kumpa kipigo cha haja Frank kwa magongo waliyonayo na wengine k" at Dar es Salaam, Tanzania - 1847753613281883422

MAPIGO YA MOYO 30 Bila kuchelewa, wale wengine walianza kumpa kipigo cha haja Frank kwa magongo waliyonayo na wengine kumcharanga sehemu kadhaa na mapanga. Dakika mbili tu zilitosha kumuacha Frank akiwa hoi pale chini. “ukome kufuata wake za watu.” Aliongea yule mwarabu na kuondoka na kundi lake huku Neila akiwa amemlalia asishuhudie tukio alilofanyiwa Frank. Kipigo walichompa Frank kilimfanya apoteze fahamu. Aliokotwa na wasamaria wema waliokuwa wakipita eneo hilo na kumpeleka hospitali. Taarifa za kuumizwa kwa mtoto wao wa pekee ziliwafikia wazazi wa Frank na kwenda mbio hospitali waliyoelekezwa kuwa Frank yupo. “vipi hali yake Dokta.” Aliuliza mama yake Frank baada ya kumuona daktari aliyekuwa ana muhudumia Frank. “hali sio nzuri sana. Kwakua amepigwa sana maeneo ya kichwani, ndio sababu itakayomfanya kuchelewa kupata fahamu.” Aliongea daktari na kuwaangalia wazazi wa Frank walioonyesha kuchanganyikiwa. “sasa baba unatusaidiaje?” aliongea mama yake Frank kinyonge “kina kipimo cha bodymass index ndio tunachoenda kumpima muda huu ili tujue mwili wake mzima umepata majeraha kiasi gani.” Aliongea Daktari na kuingia kwenye chumba alichotaka kuingia awali. Wazazi wa Frank walirudi kwenye benchi kusibiri majibu ya kipimo hicho. “mwanangu sijui kama atapona.” Aliongea mama yake Frank na kuanza kulia. “mmh mke wangu. Unajichulia ukifanya hivyo. Chamsingi ni kumuombea dua apone na kuwa mzima kama zamani.” Aliongea baba yake Frank na kumbembelea mkewe. Masaa manne baadae, Daktari aliwaita na kuwapa majibu wazazi wa Frank. “majibu yanasema kuwa amevunjika mbavu mbili za kushoto kutokana na kupigwa na kitu au vitu vizito. Kubwa zaidi ni kuwa damu imevuja kwenye fuvu lake la kichwa. Cha kuchukuru mungu ni kwamba damu hiyo haijachanganyika na ubongo. Maana ingekuwa hivyo tungekuwa tunaongelea habari nyingine hapa. Nimewaita ili msaini kama mnakubali mtoto wenu afanyiwe operation kubwa ya kichwa ili tunusuru maisha yake.” Aliongea Daktari na kumfanya mama yake Frank kuanza kulia. Baba yake Frank aliamua kuanguka saini yake na Frank akapelekwa kwenye chumba maalumu cha kufanyia upasuaji. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 24

Aliongea Lulu kwa uchungu na kuondoka huku analia. Farnk hakujali, alitoka na kufunga mlango wake na " at Dar es Salaam, Tanzania - 1844954677936719612

MAPIGO YA MOYO 24 Aliongea Lulu kwa uchungu na kuondoka huku analia. Farnk hakujali, alitoka na kufunga mlango wake na kuchukua simu yake na kutafuta jina lililoandikwa NEILA na kupiga. “ kama masihara mpenzi wangu, wiki ijayo tunarudi tena mjengoni.” Aliongea Frank baada ya salamu. “umeona eeh.. nilivyokumiss naona wiki yenyewe nyingi.” Aliongea Neila na kumfanya Frank atabasamu. “unarudi lini huko bagamoyo angalau hata nikuone kabla ya kwenda chuo?” aliuliza Frank huku akigalagala kitandani kwa utamu wa kuongea na Neila mwenye sauti ya ushawishi wa kutamani kuongea nae muda wote hata kama huna cha maana unachotaka kuongea nae. “ sirudi Dar, yaani nikitoka huku naonganisha moja kwa moja chuo.” Aliongea Neila kwa sauti ya kudeka. “haya , nilikuwa nakusalimia tu. Si unajua mimi ni mgonjwa wa sauti yako. Kila muda natamani kuisikia tu.” Aliongea Frank na kutabasamu. “kama kila muda unatamani kuisikia, nikuambie ufanye nini?” aliongea Neila na kumfanya Frank akae kwa umakini na kusikiliza kitu atakachoambiwa. “ hebu niambie basi.” Aliongea Frank kwa pozi na yeye za kisharo. “chukua simu yako record sauti yangu. Kila ukitaka kuisikia utakua unasikiliza muda wote.” Aliongea Neila na wote wakacheka. Siku ilipowadia Frank alifika chuoni mapema na Neila akafika siku inayofuata. Hakika kila mmoja alionekana kummiss mwenzake. Walikumbatiana na kupigana mabusu yasiyo na idadi. Frank na Neila walikua wapenzi waliopendezana na watu wote waliowaona walikiri kuwa walikua wanaendana. Mwili wa Frank ulifutuka na kuwa zaidi ya alivyokuwa mwanzo. Alirudi tena gym na kutengeneza mwili wake vizuri Kutokana na huo ndio ulikuwa mwaka wa mwisho pale chuoni. Frank aliandikwa kwenye kumbukumbu za wanafunzi waliokipa chuo mafanikio makubwa na kukitangaza hadi nje ya nchi kutokana na kiwango cha hali ya juu alichonacho Frank kama mchezaji wa mpira wa miguu. Yote hayo yaliwezekana kwakua alikua amempata mwanamke aliyeumiza hisia zake kwa muda mrefu. Walimaliza mitihani yao ya mwisho na kurudi makwao. Lakini Neila hakurudi na Frank kama Frank mwenyewe alivyotarajia. Alichukuliwa na mtu aliyekuja na Land rover na kuondoka naye. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 19

Walitafuta jina la Neila na baada ya kumuona alicheka.
“sio mbaya lakini, ameshika nafasi ya 6.” Alio" at Dar es Salaam, Tanzania - 1841535295751567754

MAPIGO YA MOYO 19 Walitafuta jina la Neila na baada ya kumuona alicheka. “sio mbaya lakini, ameshika nafasi ya 6.” Aliongea kwa Dharau baada ya kuona kampita masomo yote tena kwa point nyingi. “hongera, umekuwa mtu wa 6.” Aliongea Frank baada ya kumuona Neila amejiinamia. Neila alinyanyuka akiwa na sura nyingine tofauti na ile aliyoizoea. Hali iliyomfanya Frank ashangae. “ hapa shuleni kila mtu ameletwa na mzazi wake, so matokeo yangu hayakuhusu. Ni nani amekuambia alikua anahitaji umuangalizie matokeo yake?.. kuongoza mitihani isiwe shida kwa wengine. Siku nyingi sana nilikua siipendi tabia yako ya kujisikia ndio maana nikakwambia ufute yako. Nikafikiri umejirekebisha kumbe ndio tabia uliyozaliwa nayo. Unafikiri sijakusikia ulipokuwa unajitamba eti nilifikiri nimepata mpinzani kumbe yule dada boya tu… acha shobo mtotoo wa kiume, fuata yako halafu tusijuane coz tumekutana chuoni tu hapa.” Maneno yale ambayo yalisika na umati mkubwa waliokuwa pale kutokana na Neila kuongea kwa nguvu, ndio kulikomfanya aumie sana rahoni na kupata aibu kubwa. Furaha yote aliyokuwa nayo juu ya kufaulu vizuri iliyeyuka kama barafu kwenye jua kali. Aliulaumu sana mdomo wake kwa kuropoka mambo ambayo yangemshusha maksi kwa Neila. Tukio hilo lilimkosesha raha Frank. Hakupenda kumchukiza Neila hata kidogo. Alijua kuwa kumuuzi binti huyo ni sawa na kujipa adhabu kali inayomuumiza mwenyewe. Urafiki ukafa kinamna hiyo. Hakukua na salamu wala maongezi yoyote kati yao. Awapo Frank sehemu yoyote, basi Neila hakusogeza miguu yake pale. Na hata kama Neila alikua anapiga story na watu mbali mbali, basi akija tu Frank yeye huondoka eneo hilo. Unyonge mkubwa ulimpata Frank na kujiona kuna kitu anakosa kutoka katika maisha yake. Alijiridhisha kwa kuwachukua marafiki wa karibu wa Neila na kutembea nao. Hiyo ndio ilizidi kumpunguzia maksi Frank na kuzidi kuchukiwa na Neila. Uwezo wake wa kusakata kabumbu ulipungua kiwango siku hadi siku. Kuna wakati hakua msaada kabisa kwa timu yao ya chuo. Kocha wao alimuita na kumuuliza ni nini tatizo. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 17

Siku zilikatika bila Lulu kuonana na Frank mpaka siku ambayo Frank alikua anarudi tena chuo.
“wewe mw" at Dar es Salaam, Tanzania - 1841211612126414677

MAPIGO YA MOYO 17 Siku zilikatika bila Lulu kuonana na Frank mpaka siku ambayo Frank alikua anarudi tena chuo. “wewe mwanamke, huchoki wala huelewi ukiambiwa kitu. Sikupendi na sikuhitaji hata bure katika maisha yangu. Niseme na kitu gani ndio unielewe?” aliongea Frank baada ya kumuona Lulu akimfata wakati alipokuwa ana paki mabegi yake kwenye gari. “Frank, najua hujui mazito yanayonikabili ndani ya mtima wangu. Kila kilichokuwa kwenye mwili wangu nilikupa password zake na ulizifungua utakavyo. Nimekupa mpaka uhuru wa kuingia kwenye ikulu yangu yenye thamani zaidi ya falme za kiarabu. Si mimi Frank ambaye sichoki dharau zako na kukubali kama hunipendi. Tatizo ni moyo Frank. Moyo wangu ndio hausikii wala haoni juu yako. Macho yangu hayaoni kwa wanaume wengine na kukuona wewe tu. Maumivu unayonipa yanapoozwa na sura yako tu ingawaje kauli zako ni mzigo mkubwa uliomulemea kizee jangwani na asiyekuwa na msaada wowote Frank.” Aliongea Lulu huku machozi yanamtoka. “Frank tazama machozi yangu angalau kwa jicho la huruma nipate japo faraja. Kwani idadi ya matone ya machozi yangu hayafanani na uzito wa maumivu ya moyo yanimalizayo mwili kila kukicha. Sihitaji kujua nitakuwa nafasi ya ngapi kati ya uwapendao. Ile kunikaribisha hata nje ya moyo wako nitafarijika. Bora uongo utakaonipa faraja kuliko ukweli utakaoniumiza. Nakupenda Frank zaidi ya niwezavyo kukuelezea.” Maneno ya Lulu yalipita kama upepo masikioni mwa Frank. Alimtazama na kuyapokea maua aliyoletewa na kuingia nayo kwenye gari. “nimekuelewa, nitakujibu nikipata likizo nyingine.” Hayo maneno ya Frank kidogo yalimpa faraja Lulu. Baada ya hapo safari ya kuitafuta ubongo kwa ajili ya safari ya Dodoma kuendelea na masomo yake ilianza. #storynzuriiplanet_com HAPPY BIRTHDAY @deedaylan YOUNG LION @diamondplatnumz@hamisamobetto

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "PENZI LA MATESO 72

Ndio uzur wa si wanaume hata tukosame vipi ila bado likitokea tatizo tupo pamoja. "Huyu atakufa sio " at Dar es Salaam, Tanzania - 1834707765900044049

PENZI LA MATESO 72 Ndio uzur wa si wanaume hata tukosame vipi ila bado likitokea tatizo tupo pamoja. "Huyu atakufa sio bureee ngoja" Haraka alizunguka upande wa pili na kuingia chumban mle alimshika chiku ila ilikua ni kazi ngumu kumfanya atoe mkono wake kuachia dudu ile. Baba sekela aliona anawachezea. Alimnyoosha ngumi moja ya shavu mbona chiku aliachia mwenyewe na kutua pembeni. Meno mawili kuleee dam tu ndizo zilizotawala mdomo wake. Ila bado hakukaa kimya aliinuka na kutaka kumdaka tena mudi ila baba sekela aliwahi kumdaka. "Nawe unashangaa nini vaeni nguo mtoke atawaua huyuu" Ndio aliwashtua na haraka walivaa nguo na kutoka mbio huku mudi akichumbagila kama zombie. Chiku aliparangana na baba sekela pale kuona haachiwi aliamua kuanza kumtemea damu zile zilizokua zinamtoka mdomoni. Baba sekela alimsukuma na kuwahi kutoka kisha alifunga mlango kwa nje. Hiyo ndiyo ikawa njia ya kutuliza ugomvi ule. Anitha na mudi kila Mtu Alikimbikia kwake. Mudi alienda kwa rafiki yake huku anitha akienda nyumbani alikokua anakaa. Baada ya mudi kufika kwa rafiki yake bahati nzuri alimkuta maana bado ilikua ni asubuhi. "We jamaa vipi mbona unatembea kama umetoka kutairi hivi" "We acha tu jamaa yangu" Mudi aliingia ndani na kuvua suruali yake haraka kisha kuangalia usalama wa dudu yake. Ase maumivu yalikua ni makubwa sana aliyokua anayapata. "Mbona ckuelew jamaa yangu umefika na kuanza kuvua suruali tu. Ilibidi mudi bila kuficha amsimulie rafiki yake. "Ohoo mi nilishakwambia kuoa ndio nn si unaona sasa matatizo yake ndio kama haya afu nawe unakosea sana kwa nini utembee na mdogo wake tna humohumo geto na mkeo yupo" Rafiki yake alimsema sana ila mudi hakuona kosa kabisa "Kwani kuna ubaya bwana mi nampenda yule mdogo wake basi" "We nawe ni lijinga LA mwisho haya poa Fanya upendavo we" Rafiki wa mudi aliamua kumuacha tu mudi afanye awezavo "Mi nitakua hapa kwa mda huku nikiwaza LA kufunya tu" Aliamua kujipumzisha kwa rafiki yake ajue afanye nn kama kuyavuruga alishayavuruga. #storynzuriiplanet_com SIMULIZI ZA SAUTI SOON