Online Instagram Content Viewer sGeneralsta
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea hashtag

Posts attached with hashtag: #itaendelea

Dominick Salamba (@dominicksalamba) Instagram Profile Photodominicksalamba

Dominick Salamba

 image by Dominick Salamba (@dominicksalamba) with caption : "UCHAMBUZI WA MECHI YA AZAM Fc VS SIMBA part 1.
.
.
AZAM FC
Kuelekea mchezo wa leo Azam Fc itahitaji kupata matokeo ili k" - 1984754912194275328
ReportShareDownload568

UCHAMBUZI WA MECHI YA AZAM Fc VS SIMBA part 1. . . AZAM FC Kuelekea mchezo wa leo Azam Fc itahitaji kupata matokeo ili kupunguza gap kwa Simba na kuweza kuwasogelea Yanga katika mbio za ubingwa Tpl pia itahitaji kushinda ili kufuta makosa ya michezo ya nyuma kwa sababu katika mechi 2 zilizopita Azam fc imeambulia alama 1. MECHI 2 ZILIZOPITA ZA AZAM FC TPL. _Tz.Prisons 1-0 Azam❌. _Coastal union 1-1 Azam➗. UCHAMBUZI _Azam ni timu ambayo katika msimu huu kikosi chake kimekusanya nyota bora zaidi mfano: Mudathir Yahya,Sure boy,Chirwa,Singano,Ngoma ambao wana uwezo binafsi lakini pia kwa ujumla wake wana uwezo wa kuamua matokeo. _pia Azam fc wana makocha bora ukimuangalia Hans van Plujm na msaidizi wake Juma Mwambusi ni walimu wanaojua kuusoma mchezo lakini pia Azam Fc ni timu yenye facilities nzuri kwa hiyo hivi karibuni wanavyofanya vibaya waalimu na wachezaji wanapaswa kulitazamia hili lakini hawawezi kusingizia facilities. _pia Azam fc ni wazuri sana katika umiliki wa mpira na ina wafungaji wazuri mfano Donald Ngoma,Dani Lyanga,ObreyChirwa,Mahundi _Tofauti ambayo wanayo Azam Fc inaonekana ni timu ambayo imekosa muendelezo pia ni timu ambayo imekosa muunganiko kuanzia Eneo la beki--kiungo-- ushambuliaji na tatizo linaanzia wakati Azam fc ikiwa haina mpira maana yake ikianza kushambuliwa unaona hakuna muunganiko mzuri kati ya viungo na mabeki. #Itaendelea....... __.

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photovennita_mwita

Vennita Mwita

 image by Vennita Mwita (@vennita_mwita) with caption : "#Kosa_langu #Hadithi_inaendelea
#Sehemu_ya_8 ........Mama Emma aliniogesha na kunivalisha nguo za mwanae, akaniambia kuw" - 1981294197264837139
ReportShareDownload264

#Kosa_langu ........Mama Emma aliniogesha na kunivalisha nguo za mwanae, akaniambia kuwa hiyo ilikuwa siku ya mazishi ya mama yangu hivyo nijitahidi, nijikaze ili niweze kumuaga mama yangu kabla hajazikwa. Sikuelewa. Moyoni mwangu niliamini ningeondoka na mama yangu kwenda huko mbinguni, sikumjibu kitu mama Emma zaidi ya kuendelea kulia tu. Kabati kubwa lililetwa nyumbani kwetu, watu walisimama na wengine walilia sana, kabati lilipokelewa na kina baba na kuwekwa juu ya meza iliyokuwa tayari. Kulikuwa na msalaba mkubwa mweupe. Watu wote walikuwa kimya, nilikaa karibu na mama Emma. Nami nililia, sikuelewa kila kilichotendeka. Mama Emma aliniambia lile lilikuwa jeneza la mama yangu, ilitupasa kuaga mwili na kwenda kuzika makaburini; kwa mara ya kwanza ganzi ilinibana kuanzia miguuni hadi kichwani. Nilihisi kuzimia, kwa takribani dakika kadhaa sikujua niko wapi. Nilishitushwa na kelele za vilio vya kina mama waliopita mbele ya kabati la mama yangu! Sikuwa mbali, nilimuona mama yangu akiwa amelala vyema, lakini mweusi kidogo, moyoni mwangu niliita mamaaa; amka mama yangu, amka ukae na mimi mama; haikusaidia kwani mama hakuamka. Nilifumba macho yangu, machozi yakinitoka, niliiona taswila ya mama yangu ikitabasamu kwa machozi mbele yangu, nilitamani mama anibebe, oh! Nilipofumbua macho sikumuona mama yangu mbele yangu, bali mwili wake ndani ya kabati. Mama yangu kalala usingizi. Mama yangu ninaye mpenda hataki nimuamshe,yupo katika ndoto ndefu! "Mama yangu amkaaaa! amkaa mama yanguuuuu! amkaaaa, mamaaa! Nitaishi na nani mamaaa? Nitaishi wapi mimi mama, nitakula nini? Nguo za shule zimechanika mama, amkaaaaa!" Nilimshika mama yangu nilipopita mbele ya jeneza, nililia sana, nilimuita mama pasipo mafanikio yoyote, mama hakufumbua hata jicho lake moja. Alikuwa wa baridi kama barafu. Oh, mama yangu! Nilitolewa pale na mama Emma ambaye nae alilia sana, watu wote wake kwa waume walilia pindi nilipoaga mwili wa mama yangu..... #Itaendelea........ #Mtunzi: Vennita Mwita @vennita_mwita @vennita_mwita

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photovennita_mwita

Vennita Mwita

 image by Vennita Mwita (@vennita_mwita) with caption : "#Kosa_langu #hadithi_inaendelea 
#Sehemu_ya_7 ........ Tuliondoka kwenda nyumbani kwa haraka, nilikimbia na kuwa wa kwan" - 1980744570945882959
ReportShareDownload448

........ Tuliondoka kwenda nyumbani kwa haraka, nilikimbia na kuwa wa kwanza kufika, nilikuta bado mama kalala vilivile, nililia pia. Kina mama Emma walipofika nyumbani waliingia ndani moja kwa moja. Walilia kwa sauti na kumshikashika mama, sikuelewa. Majirani toka pande zote walianza kuja pale nyumbani. Nilijua mama yangu amezidiwa, nitapata wapi pesa ya kumpeleka mama hospitali au je majirani watanichangia? Sikujua nifanye nini. Walitaka kujua hali ile imetokea lini, nami nikawambia jana mchana, yaani jumapili, na nililala na mama akiwa hivyo, mpaka leo hajamka. Nilitaka wanisaidie kumuamsha mama yangu kisha wao waondoke zao! Nimemzoea mama yangu na ni mtu pekee ninaempenda sana na ninaetaka kuishi naye, nataka aamke! Watu wengi zaidi walijaa nyumbani, Mama Emma aliniambia kuwa mama yangu amefariki, sikuelewa. Nilimuuliza anahitaji dawa gani ili aweze kuamka, au je achomwe sindano? Mama Emma aliniambia kuwa mama yangu hataamka tena, na inabidi azikwe kaburini, sikuelewa. Kwanini mama asiamke? "Mama yako amekwenda mbinguni" alinijibu mama Emma na kusema watu wakienda mbinguni hawarudi tena dunuani na miili yao huzikwa kwenye shimo na kufukiwa na udongo! Sikuelewa! Ila sikutaka mama yangu afukiwe kwa udongo kwani bado namuhitaji. Kilipikwa chakula, watu walikula ila mimi sikuweza! Watu wengi walikuwa wakiuliza mtoto wa marehemu yuko wapi, na kila aliye niona alitokwa machozi, hasa wakina mama. Sikuelewa haya yote. Mama yangu alipelekwa hospitalini kuhifadhiwa, niliamini atakuja akiwa amepona! Ilitangazwa mama angezikwa siku iliyofuata, katika makaburi ya Buguruni Malapa. Nami niliamini basi nitazikwa na mama yangu, kamwe nisingeacha azikwe peke yake wakati ni yeye tu aliyenipenda, ni mtu pekee aliyenijali mimi. Mipango ya mazishi ilipangwa. Sikuwa na mtu niliyemfahamu au ndugu wa karibu, zaidi ya marafiki wa mama yangu aliofanya nao biashara sokoni boma. Nililia usiku na mchana, sikuongea na mtu, niliomba nikamuone mama yangu hospitalini lakini hakuna aliyenipeleka. Nililazimishwa kula lakini sikuweza... #Itaendelea...... #Mtunzi Vennita Mwita @vennita_mwita

Foc Entertainment Media (@foc_media) Instagram Profile Photofoc_media

Foc Entertainment Media

 image by Foc Entertainment Media (@foc_media) with caption : "KISUKARI HUSABABISHA 1.UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, 2........ Mamilioni ya WaTanzania wanaendelea kujipatia Kitabu hiki i" - 1980514138310156446
ReportShareDownload06

KISUKARI HUSABABISHA 1.UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, 2........ Mamilioni ya WaTanzania wanaendelea kujipatia Kitabu hiki ili kupata Suluhisho na maarifa zaidi juu ya Kisukari. Wasiliana na Nestory John ujipatie Nalala yako sasa popote ulipo. #Itaendelea

Ujue Moto (@ujuemoto) Instagram Profile Photoujuemoto

Ujue Moto

ReportShareDownload451

_ Wapo baadhi ya Madereva wanaweka fire extinguisher kwa sababu ya kuogopa Askari na si Usalama wa Gari. Angalia hii video fire extinguisher haifanyi kazi wanahaha hawajui la kufanya. #ITAENDELEA #Tag_Marafiki _ #Kagua_Fire_Extinguisher_Yako #Hakikisha_Gauge_Iko_Full #Wasiliana_Nasi_kwa_Service _ #Jionee_Tofauti Jifunze na @UjueMoto 🔍#Instagram /#Facebook_Page /#YouTube #Like, #Follow & #Subscribe _ #HUDUMA_ZETU: > #Tunauza, #Tunafunga na #Kukarabati vifaa vya Moto > #Tunatoa Ushauri wa Kitaalam kuhusu Usalama wa Majanga ya Moto _nk. #Ushauri_BURE _ #MAWASILIANO_YETU: 📞0736 - 237 134 📞0655 - 237 134 📧 ujuemoto@gmail.com 📌 Tabata Mangumi-Segerea Rd _ #Majanga_ya_Moto_Yanaepukika

🔝90sports_plus🔝 (@90sports_plus) Instagram Profile Photo90sports_plus

🔝90sports_plus🔝

 image by 🔝90sports_plus🔝 (@90sports_plus) with caption : "Via - @dominicksalamba .
.
TATHIMINI KUELEKEA MECHI YA YANGA NA SIMBA. PART I.
.
Kwanza mchezo huo utachezwa katika uwan" - 1980021850331347899
ReportShareDownload2181

Via - @dominicksalamba . . TATHIMINI KUELEKEA MECHI YA YANGA NA SIMBA. PART I. . Kwanza mchezo huo utachezwa katika uwanja wa taifa Dar Es Salaam majira ya saa 10:00 jioni. . . TUANZIE NA YANGA. .... Yanga mpaka sasa wameshinda michezo 18 wamepata sare 4 na kufungwa mchezo 1 na wanaongoza ligi kuu Tanzania Bara. ..... 1.UBORA WA KOCHA. _Kocha Mwinyi Zahera ana uwezo Wa kuunganisha wachezaji pia ana uwezo wa kuusoma mchezo kabla ya mchezo na wakati wa mchezo ukiwa unaendelea pia amekuwa na uwezo wa kufanya mabadiliko ambayo yanaleta impact ambapo hadi sasa Mwinyi zahera asilimia 90 ya mabadiliko aliyoyafanya msimu huu yameleta matunda kwa maana amekuwa akipata ushindi,au Uhitaji Wa sare ,au kulinda ushindi kupitia mabadiliko ambayo anayafanya pia. _pia kocha Zahera ameweza kutengeneza uwiano sawa kwa wachezaji wa kikosi cha yanga kwa maana rotation anayokuwa anaifanya Mara nyingi imekuwa ikimpatia matokeo kwa hiyo katika mchezo dhidi ya Simba kuna uwezekano mkubwa kwa wachezaji wa yanga kupata matokeo endapo wakimsikiliza mwalimu wao. ..... 2.MAPUNGUFU KIKOSI CHA YANGA. _Safu ya ulinzi ya Yanga imekuwa ikifanya makosa sana hasa katika mipira ya krosi Kabwili pamoja na Kindoki wamekuwa wakifanya makosa sana. _pia safu ya ulinzi ya Yanga wanaposhambuliwa one against one mabeki wa yanga wamekuwa wakipaniki sana kitu ambacho kinapelekea kuigharimu safu ya ulinzi na timu nzima kwa ujumla mfano:Yondani,Andrew Vicent na Shaibu kuelekea mchezo dhidi ya Simba wanatakiwa wajiangalie. #itaendelea.

sunday school moravian moro (@watumishi_choir) Instagram Profile Photowatumishi_choir

sunday school moravian moro

 image by sunday school moravian moro (@watumishi_choir) with caption : "UNAYO NAFASI NA WAJIBU WA KUWARITHISHA WATOTO WAKO IMANI "ISIYO YA KINAFKI"... 2 Timotheo 1:1-5 "........Nami natamani s" - 1977601757191066350
ReportShareDownload05

UNAYO NAFASI NA WAJIBU WA KUWARITHISHA WATOTO WAKO IMANI "ISIYO YA KINAFKI"... 2 Timotheo 1:1-5 "........Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaaa kwanza kwa bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo....." #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 98
MTUNZI:EDO MAN  Binti yangu! Ibrahim alinihadithia kila kitu kuhusu wewe hata kabla hajajua kam" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975971641394973838

HADITHI:MREMBO LATIFA 98 MTUNZI:EDO MAN Binti yangu! Ibrahim alinihadithia kila kitu kuhusu wewe hata kabla hajajua kama mimi ni mzazi wako, naomba umsamehe, inawezekana mambo yote anayopitia, shida zote anazozipata ni kwa ajili ya laana yako, msamehe na sahau kila kitu,” alisema mzee Deo. Latifa akayapeleka tena macho yake kwa Ibrahim, alipanga kutokusamehe katika maisha yake lakini kila alipokuwa akimwangalia, bado mwanaume huyo alionekana kuhitaji msamaha. Alionekana kupigika katika maisha yake, alitia huruma lakini pamoja na hayo yote, alifanya kazi kubwa sana kumlea baba yake. Hakuwa na fedha za kutosha lakini nkiasi hichohicho kidogo alikitumia kwa ajili ya kumtibu baba yake, hakika alifganya jambo kubwa lililohitaji sifa kubwa kutoka kwake. Hakuongea kitu, alichokifanya ni kumsogelea na kumkumbatia. Wote wawili walikuwa wakibubujikwa na machozi. Latifa hakuwa na jinsi, aliukana moyo wake na kumsamehe mwanaume huyo aliyeonekana kuhitaji sana msamaha. “Nisamehe Latifa.” “Nimekusamehe Ibrahim, Ahsante kwa yote uliyomfanyia baba yangu,” alisema Latifa huku akijifuta machozi. “Naomba umsamehe Nusrat pia! Ni mwanamke mpumbavu asiyejua lile analolifanya. Naomba umsamehe.” “Nimsamehe Nusrat?” “Ndiyo! “Kwa hivi alivyomfanyia baba yangu? “Latifa! Hebu sahau kwanza. Wewe ni mtu mkubwa na mwenye heshima, tazama dunia nzima inakutazama wewe, usiposamehe, vipi wale vijana wanaotaka kuwa kama wewe? Nao watakapokosewa hawatakiwi kukosea kisa wewe haukusamehe? Vipi kuhusu wale watoto wanaotaka kuwa kama Latifa, kweli nao hawatakiwi kusamehe? Samahe saba mara sabini, au umesahau hilo?” aliuliza Ibrahim. “Nakumbuka.” “Basi naomba umsamehe!” “Nimemsamehe!” “Nashukuru!” Huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha mapya, Latifa hakuwa na kinyongo, moyo wake ulilainika na hakutaka kuwa na kingo na mtu yeyote yule, alichokiamua ni kumsahmehe kila mtu aliyewahi kumfanyia ubaya kwa makusudi au bahati mbaya. Alikuwa mtu mwenye mafanikio, bilionea, alichokifanya ni kumsafirisha baba yake nchini Marekani, alitaka akatibiwe huko na kuishi naye hukohuko. Kwa Ibrahim, japokuwa alimfanyia mambo mabaya nyuma hakutaka kumuacha hivihivi, aliamua kumsaidia kama alivyomsaidia baba yake. #itaendelea

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photovennita_mwita

Vennita Mwita

 image by Vennita Mwita (@vennita_mwita) with caption : "#Kosa_langu _sehemu _ya_5 .............. ‘Sifa ya mtoto wa kiume ni kujikaza, usilie Paul, kuwa jasiri, unabaki ulimweng" - 1975706600169839772
ReportShareDownload362

_sehemu _ya_5 .............. ‘Sifa ya mtoto wa kiume ni kujikaza, usilie Paul, kuwa jasiri, unabaki ulimwenguni hapa peke yako, huna wazazi wala ndugu wa kuzaliwa nae, wala Ndugu yangu unayemfahamu, kuwa jasiri kuitazama hii dunia, wewe ni mwanangu mzuri na jasiri, kweli Paul?’ ‘Ndio mama,’ nilijibu na kufuta machozi, lakini sikuelewa! ‘Vizuri’ alijibu mama kisha akinibusu kichwani na mkononi, akasema kwa sauti ndogo sana na kwa shida, ‘kwaheri Paul’ akalala. Nilipoona mama amelala kwa muda mrefu, na amekuwa wa baridi sana, nilifurahi na kuhisi mama anakaribia kupona, niliamka na kula mandazi na juisi. Baada ya kula niliona mama kalowa jasho mwili mzima, nilimtoa nguo zake, nikaloweka kitambaa kwenye ndoo na kuanza kumfuta kwani alinifanyia hivi mimi nilipoumwa homa, kisha nilimufunika kanga, sikutaka kumuamsha kwani alionekana amechoka sana. Nililala tena ubavuni mwake na kuwaza ni lini mama yangu atapona. Tulilala kwa muda mrefu sana. Nilipoamka jioni niliona mama bado kalala, hakugeuka wala kupumua, ‘mama amechoka kweli’ nilisema. Nilienda kuchota maji bombani kisha nilimuamsha mama ili aoge kwani alikuwa na jasho tena! Mama hakuamka, nilimuaga ili nikatafute chakula cha jioni sokoni, lakini pia mama hakuamka! Ilibidi niende. Nilifanikiwa kupata makande kwa mteja wa mama wa chakula, aliponiuliza mama anaendeleaje nilimwambia kuwa mama kalala na anaendelea vizuri sana..... #Itaendelea..... #Fb: Vennita Mwita : Vennita Mwita #Mtunzi: Vennita Mwita

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 92
MTUNZI:EDO MAN 
Ibrahim akamchukua mzee Deo na kwenda kutulia naye kochini, akachukua rimoti ya" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975301072798282220

HADITHI:MREMBO LATIFA 92 MTUNZI:EDO MAN Ibrahim akamchukua mzee Deo na kwenda kutulia naye kochini, akachukua rimoti ya televisheni na kisha kuiawasha. Mzee Deo alikaa kitini, hakujisikia kuangalia, hakuwa na amani kabisa kwani jinsi alivyokuwa akimwangalia Nusrat ambaye alikaa pembeni kabisa, alionekana kuwa na hasira mno. Latifa alivyoonyeshwa kwenye televisheni, Ibrahim akajikuta akianza kububujikwa na machozi, moyo wake uliumia, kila alipokuwa akimwangalia msichana yule, akagundua kwamba aliitupa almasi jangwani na kuokota bati. Msichana huyo mrembo, mwenye muonekano wa fedha akaanza kusimulia historia ya maisha yake. Kila mmoja akabaki kimya akimsikiliza, alianza kusimulia kuanzia mbali, tangu mama yake alipofukuzwa nyumbani kwao, alipokwenda nyumbani kwa mpenzi wake, Deo kisha kumfukuza, alionekana kuumia mno. Mzee Deo aliposikia historia aliyokuwa akiisimulia Latifa, akashtuka, akaanza kumwangalia Latifa, akasimama kutoka katika kochi lile na kuisogelea televisheni, kila mmoja mule ndani akabaki akimshangaa. “Ibrahim….” aliita mzee Deo, machozi yakaanza kumtoka. “Nipo mzee….” “Latifa ni binti yangu!” alisema mzee Deo huku akionekana kushangaa, Ibrahim akashtuka, si yeye tu, hata Nusratakashtuka. “Unasemaje?” “Kumbe Latifa ndiye mtoto wangu aliyezaliwa na Nahra,” alisema mzee Deo. Hapo ndipo Ibrahim alipoanza kukumbuka mahojiano yale, alikumbuka Latifa alimtaja mtu aliyeitwa Nahra na Deo, wazazi wake waliokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mpaka baba yake alipomfukuza mama yake. Mahojiano yale akayaunganisha na historia aliyowahi kusimuliwa na mzee huyo kwamba zamani alikuwa na mwanamke wa Kihindi, alimpa ujauzito lakini baadaye akafukuzwa nyumbani kwao, na alipokuja kwake, naye alimfukuza ila ni kwa sababu tu alitishiwa kuuawa na ndugu zake Nahra kwa kutumiwa watu waliokuwa na bunduki, na kama asingemfukuza basi angeuawa yeye. “Ni mtoto wangu! Kumbe Latifa ni mtoto wangu!” alisema mzee Deo huku akijifuta machozi. Ibrahim alishindwa kuamini, wakati mwingine alifikiri kwamba alikuwa ndotoni, katika kipindi chote alichokuwa akiishi na huyo mzee, alivyokuwa akizungumza naye kumbe alikuwa mzazi wa msichana aliyekuwa amemuacha, Latifa. #itaendelea